Muuguzi ambaka mama mjamzito

Muuguzi ambaka mama mjamzito

Jeshi la polisi mkoani Tabora linamshikilia Rayson Agnelusi Duwe muuguzi msaidizi katika hospitali ya wilaya ya Sikonge, kwa kosa la kumbaka mama mjauzito wa miezi tisa baada ya kumchoma sindano yenye dawa ya usingizi.

ACP. Richard Abwao akitoa taarifa ya tukio hilo ambalo amelitaja kuwa sio la kiungwana amesema lilitokea June 9, 2023 majira ya saa mbili usiku.

Aidha kamanda huyo amesema muuguzi huyo ambaye aliingia kazini akiwa amelewa pombe alitenda kosa hilo wakati alipopangiwa zamu ya usiku ya kuhudumu wagonjwa wa nje (OPD) ndipo alipotoka na kwenda chumba cha wagonjwa wa ndani na kumbaka mama huyo mwenye ujauzito.

Samabamba na muuguzi huyo kukutwa na bomba la sindano pamoja na dawa za usingizi huku taarifa ya kitabibu zikithibitisha kuwa alimwingilia mama huyo mwenye ujauzito.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags