Murphy kuonekana kwenye Peaky Blinders

Murphy kuonekana kwenye Peaky Blinders

Baada ya kuondoka na tuzo ya Oscar 2024, kama Mwigizaji Bora wa Kiume, Cilian Murphy ameripotiwa kuonekana katika muendelezo wa filamu ya ‘Peaky Blinders’.

Taarifa hiyo imethibitishwa na muandaaji wa filamu hiyo Steven Knight, ambapo alieleza kuwa ameamua kumchagua mkali huyo kutokana na kipaji alichonacho huku akiweka wazi kuwa anastahili kuwa kwenye filamu hiyo.

Filamu hiyo itaelezea familia ya Tommy na genge la ‘Peaky Blinders’ katika vita ya kwanza ya dunia. Inatarajiwa kuanza kurekodiwa September mwaka huu na Murphy atacheza uhusika wa Tommy Shelby.

Cillian Murphy ameonekana katika filamu mbalimbali zikiwemo ‘28 Days Later’, ‘The Delinquent Season’, ‘Red Eye’, ‘The Wind That Shakes the Barley’ na nyinginezo.

Mkali huyo wa ‘Oppenheimer’ amewahi kupokea tuzo nyingine kama ile ya ‘#Academy’, ‘Golden Globe’, Tuzo ya #BAFTA. Kwa upande wa tuzo za #Oscar hii inakuwa ya kwanza kwake.
.
.
#mwananchiscoop
#burudikanasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags