Muonekano wa ndani nyumbani kwa P Diddy baada ya Uchunguzi wa Polisi

Muonekano wa ndani nyumbani kwa P Diddy baada ya Uchunguzi wa Polisi

Video fupi iliyotolewa na mtandao wa TMZ ikionesha hali ilivyo ndani ya nyumba ya P Diddy iliyopo Miami baada ya kufanyiwa uchunguzi

Ikumbukwe siku ya juzi Jumatatu, Machi 25 yaliibuka mapya baada ya makazi yake ya Los Angeles na Miami kufanyiwa upekuzi na Mawakala wa usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.

Uchunguzi huo uliongozwa na mawakala wa Uchunguzi wa Usalama wa Nchi (HSI).

Tuhuma  za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili Diddy ni zile zilizoanza kuvuma tangu mwaka jana.

Hata hivyo, katika upekuzi huo, watoto wawili wa kiume wa Diddy, Justin na King Combs, walitiwa mikononi mwa askari.

Jumba lililofanyiwa upekuzi ni lile ambalo alizindulia albamu yake ya mwisho mwaka jana (The Love Albam Off Grid).

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya uchunguzi  huo uliofanywa, maafisa wa Polisi wameondoka na vifaa vyote vya umeme kama simu na laptop walizozikuta ndani ya nyumba pamoja na baadhi ya nyaraka

Hata hivyo watoto wake wawili King& Justine waliokamatwa Machi 25 wameachiwa huru lakini baada ya kuachiwa kurudi nyumbani  walionekana wakipakia vitu vyao kwenye magari na kuondoka.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags