Mume wa Nicki Minaj jela miaka 3

Mume wa Nicki Minaj jela miaka 3

Bwana weeeh! Mume wa rapa kutoka nchini Marekani Nick Minaj, Kenneth petty amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu chini ya Uangalizi wa Mahakama na Kifungo cha Nyumbani mwaka mmoja baada ya kukiri kushindwa kujisajili kama mkosaji Kingono (Sex Offender) Katika jimbo la California mwaka 2020

Aidha kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali, Mahakama pia imemtaka alipe faini ya Tsh. Milioni 128. Kenny alihitajika kukubali kama mkosaji wa kingono baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana wa Miaka 16 mwaka 1995.

Heyy! Una maoni kwa mwanadada huyu kwa sasa, dondosha komenti yako hapo chini na usiache kufuatilia mitandao yetu ya kujamii @Mwananchiscoop kwa habari Zaidi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags