Mume Amuua Mkewe wakiwa Fungate

Mume Amuua Mkewe wakiwa Fungate

Duuuuuh! Ama kweli mambo ni mengi muda ni mchache, kwa taarifa zinazo samba kupitia mitandao ya kijamii ni kutoka kwa mwanaume mmoja lutoka Marekani kumuua mkewe wakiwa katika fungate.

Bradley Robert Dawson; mwanaume raia wa Marekani ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kumuua mkewe walipokuwa kwenye honeymoon (fungate) kwenye hoteli ya kifahari huko katika Visiwa vya Yasawa huko Fiji, Kusini mwa Bahari ya Pasifiki.

Jeshi la Polisi katika eneo hilo limethibitisha kuwa alasiri ya Julai 9, mwanamke aliyetambuliwa kuwa ni raia wa Marekani, Christe Chen mwenye umri wa miaka 36 alipatikana akiwa amefariki dunia kwenye sakafu ya chumba cha walichokodisha kwa ajili ya mapumziko baada ya kufunga ndoa.

Wafanyakazi wa hoteli hiyo waliwaambia Polisi kwamba Chen alifariki dunia baada ya kupigwa na mume wake wakiwa fungate.

Mume wa Chen aliyetambuliwa kama raia wa Marekani Bradley Robert Dawson mwenye umri wa miaka 38, alipatikana na kukamatwa siku mbili baadaye huko Nadi  Pwani ya Magharibi ya Kisiwa Kikuu cha Fiji cha Viti Levu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags