Muigizaji Wylie akamatwa kwa wizi

Muigizaji Wylie akamatwa kwa wizi

Muigizaji kutoka nchini Marekani, #AdamWylie, anadaiwa kukamatwa na polisi kwa kosa la kuvunja maduka ya Ol Target nchini humo na kuiba bidhaa katika maduka hayo.

#BurbankPD ‘timu’ inayohusika na upotevu wa maduka nchini humo imeeleza kuwa walimuona muigizaji huyo #weekend iliyopita akiiba biadhaa za #afya na #urembo na kuzipakia kwenye toroli.

Wylie mwenye umri wa miaka 39 alikamatwa na afisa usalama wa maduka kabla kutoka nje ya maduka hayo huku akiwa amebeba bidhaa hizo zenye thamani ya dolla 108.

 #AdamWylie aliwahi kucheza filamu mbalimbali ikiwemo ‘picket Fences’,Under Wraps, Into the Wood na nyinginezo.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags