Muhubiri akamatwa kwa kuwapotosha waumini

Muhubiri akamatwa kwa kuwapotosha waumini

Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia Herman Magigita mwenye umri wa miaka 60 mchungaji wa kanisa la ‘Neno’ lililopo kijiji cha Chema.

Kwa kosa la kufanya shughuli za kanisa bila kuwa na kibali cha usajili kinyume cha sheria, na kutoa mahubiri ya kuipotosha jamii na waumini wake.

Polisi walimtia nguvuni Herman ni baada ya kupokea taarifa za mchungaji huyo kuwataka waumini wake wasiende hospitali kupata huduma ya matibabu pindi wakiugua au kuuguliwa.

Badala yake wapelekwe kanisani kwake kwaajili ya kuombewa na kupata uponyaji wa magonjwa yanayowakabili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags