Mtoto wa mwaka mmoja aweka rekodi ya dunia

Mtoto wa mwaka mmoja aweka rekodi ya dunia

Mtoto wa mwaka 1 na siku 152 kutoka Ghana aitwaye Ace-Liam Nana Sam Ankrah ameweka rekodi ya dunia ‘Guinness World Records’ kwa kuwa mchoraji mdogo zaidi duniani.

Kwa mujibu wa shirika hili Ace alianza kuchora akiwa na umri wa miezi 6 huku tayari akiwa ametengeneza zaidi ya picha 20 mpaka kufikia sasa.

Hivi karibuni Ace alishiriki katika maonesho yake ya kwanza kwenye Jumba la Makumbusho la Sayansi na Teknolojia nchini Ghana, ambapo kazi zake 10 za sanaa zilioneshwa na tisa zikauzwa hapo hapo.


Mama mzazi wa mtoto huyo Chantelle Kuukua Eghan aliweka wazi kuwa wakati alipopewa jukumu la kwenda kusimamia Miss Universe 2023 ndipo akatafuta njia ya kufanya mwanae asibaki mpekwe akiwa kwenye majukumu yake, ambapo alimnunulia vifaa vya uchoraji na baada ya miezi 6 akagundua mapenzi ya Ace katika uchoraji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags