Mtoto wa MohBad kupimwa DNA, Kujua baba halali

Mtoto wa MohBad kupimwa DNA, Kujua baba halali

Baada ya kuzuka sintofahamu kuhusu baba halisi wa mtoto wa marehemu Mohbad, wengine wakidai kuwa ni mtoto wa promota Sam Larry, baba mzazi wa Mohbad ametaka mtoto huyo kupimwa DNA ili kuthibitisha hilo.

Kwa mujibu wa This Nigeria baba wa Mohbad, Joseph Aloba ameeleza kuwa lazima kufanyika DNA maana wanigeria wanataka kujua kuhusu baba halisi wa mtoto huyo na anawahakikishia kuwepo kwenye vipimo na hata kama hatokuwepo atamtuma mwakilishi ili kujua ukweli baba halisi wa mtoto huyo.

Mohbad alifariki Septemba 12 mwaka huu akiwa ameacha mtoto wa miezi mitano kwa jina la Liam, huku sababu za kifo chake bado haijajulikana, polisi nchini Nigeria wamewashikilia promota Sam Larry na Naira Marley kwa uchunguzi zaidi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags