Mtoto wa Kanye West mbioni kuachia albamu yake

Mtoto wa Kanye West mbioni kuachia albamu yake

Binti wa mwanamuziki Kanye West, North West (10) ametangaza ujio wa album yake wakati alipokuwa jukwaani na baba yake usiku wa kuamkia leo katika ‘Vultures 2 listening party’ iliyofanyika Phoenix, Arizona.

Album hiyo aliyoipa jina la ‘Elementary School Dropout’ bado haijawekwa wazi tarehe rasmi itakayoachiwa.

Ikumbukwe kuwa mwezi uliyopia North West alifanikiwa kuingia kwenye chati za Billboard 100 kwa mara ya kwanza, baada ya kufanya 'kolabo' na Baba yake ya ngoma ya ‘Talking’ na kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wenye umri mdogo zaidi kuwahi kuingia katika chati hizo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags