Mtoto wa Beyonce kusikika kwenye animation ya The lion King

Mtoto wa Beyonce kusikika kwenye animation ya The lion King

Mtoto wa mwanamuziki kutoka nchini Marekani Beyonce, Blue Ivy (11) ameripotiwa kuwa sauti yake itatumiaka kwa mara ya kwanza katika filamu (animation) ya ‘Mufasa: The Lion King’ akiungana na mama yake ambaye tayari alishapewa uhusika toka hapo awali.

Katika filamu hiyo Blue ataweka sauti ya binti Simba aitwaye Kaira huku mama yake akiigiza sauti ya mke wa Simba ambapo animation hiyo inatarajiwa kutoka Desemba 20, 2024.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Beyonce kufanya kazi pamoja na binti yake, ikumbukwe kuwa mwaka Jana Blue alizunguka na Mama yake katika ziara ya ‘Renaissance’ akiwa kama kiongozi wa dancer.

Blue Ivy, ni mtoto mkubwa wa Beyonce ambaye amempata na msanii Jay-Z.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags