Mtoto ajiua kisa kutaniwa na wanafunzi wenzake

Mtoto ajiua kisa kutaniwa na wanafunzi wenzake

Mtoto wa miaka 10 kutoka Indiana aitwaye Sammy Teusch, amechukua uamuzi wa kujiua baada ya wanafunzi wenzake kumtania mara kwa mara kuhusu meno na miwani anayo vaa.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na familia yake huku wazazi wa mtoto huyo wakidai kuwa Sammy aliamua kujiondoa uhai Mei 5, akiwa chumbani kwake kutokana na kutaniwa na wanafunzi wenzie.

Ikiongea na vyombo vya habari nchini humo familia ya Sammy ilieleza kuwa walipeleka malalamiko katika shule aliyokuwa akisoma mtoto wao kabla ya kifo chake ambapo siku hiyo Sam alivunjiwa miwani na wanafunzi wenzie pamoja na kudhihaki meno yake lakini hakukua na hatua zozote zilizochukuliwa.

#SammyTeusch, alikuwa akisoma darasa la nne katika shule ya ‘Greenfield Intermediate School’ ambapo alifariki Mei 5, mwaka huu na kuzikwa siku ya jana Jumatano Mei 15.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post