Mto Kiwira na maajabu yake

Mto Kiwira na maajabu yake

 Na Stephen Mathias

Ahh!! Wewee Niaje mwanangu karibu katika mwendelezo wa makala zetu mbalimbali zinazokujia kila siku ya Jumanne kwa uzamini wa mtu mnene @steve G.

Ukiwa kama mwanangu wa kweli ushawai kusikia mto Kiwira…..huu ni mto ambao unamaajabu mengi mto huu, upo wilaya ya Rungwe mkoani mbeya, mto huu unakadiliwa kuwa na urefu wa kilomita 15 kutokea kwenye chanzo chake.

Asili ya mto huu ni huko Mbeya maeneo ya kiwira Magereza ambapo maji ya mto huu uanzia kwenye chemichemi kutokea milimani na umwaga maji yake, katika Ziwa Nyasa.

 MAAJABU MBALIMBALI YANAYO PATIKANA KATIKA MTO HUU.

Kama unavyojua mtu wangu, Nchi ya Tanzania Imejaa na Vivutio vingi vyenye maaajabu!!!!!!! Mengi na ya kushangaza sana tukianza na hii:

DARAJA LA MUNGU  

Nikiwa nakupa mambo mazuri ya kihistoria kutoka Mbeya Tanzania Usichukulie poa, mwanangu. Daraja la Mungu ni Jiwe kubwa sana ambalo alijawai kujengwa na mtu yeyote Yule bali Mungu Mwenyewe. Daraja hilo likiwa linaanzia mwanzo wa upande mmoja hadi upande mwingine jambo lililotengeneza daraja ambalo linavukika bila matatizo yoyote yale.

NYOKA MKUBWA MWENYE VICHWA SABA

Hapo sasa mtu wangu usije ukaota tu au kuogopa sababu nimetaja nyoka. Nyoka huyu ni nyoka mwenye vichwa saba na ni Nyoka mwenye maajabu makubwa sanaaaa!!!!! Kwa mujibu wa wenyeji wa Eneo hilo wanasema Nyoka huyu kwa jina la kienyeji anaitwa Nyefuila. Inasemekana Nyoka huyu amelalia Zahabu, Jambo linaloweka upekee wa mto huu, lakini mtu wangu Usijaribu wala kuwazia zahabu hizo maana ni zahabu za majini na mashetani japo wapo wenzako kama wewe walitamani kuzichukua zahabu hizo wakaaishia kifo…Inasemekana nyoka huyu anaambatanishwa na imani za kishilikina kwamba huusika na uletaji wa Mvua…akikasilika huleta mafuriko

KWANINI NYERERE ALISHINDWA KUVUKA MTO HUO

Nyerere ni kiongozi mkubwa wa nchi…tena ni kiongozi ambaye alijivunia sana kulindwa na wazee ama dawa mbalimbali za kienyeji jambo lililopelekea akapewa fimbo yenye madawa ya kuweza kumlinda asizulike na mambo mabaya yanayokuja mbele yake…Mnamo mwaka 1970 Nyerere alitembelea mto huo, kutaka kujua Vivutio vya mto huo lakini alipofika kwenye Daraja la Mungu fimbo yake ilikidhana sana na Nyoka iliyopo chini ya Daraja hilo jambo lililomfanya kushindwa kuvuka kwenda ng’ambo ya mto huo.

KIJUNGU

Ndani ya mto huo kuna shimo lililochongwa Vizuri na Maji, shimo hilo uingiza maji kwa nguvu sana lakini hutoa Maji popole sana jambo linaloonesha kivutio kikubwa sana kwenye mto huo…..Jiwe hilo limechongwa Vizuri sana Midhiri ya Chungu cha kupikia…

Jambo lolote lililokuwa na mwanzo alikosi kuwa na mwisho na Mwisho wa makala hii ndio Mwanzo wa Makala Nyingine usisahau ku subscribe na ku like makala hii…kama unajambo lakuongeza kuhusu mto huu na maajabu yake tupia comment yako hapo@scoop Tuzungumze zaidi……






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags