Mtendaji apewa kifungo cha nje kwa wizi

Mtendaji apewa kifungo cha nje kwa wizi

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipapa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Nassim Mbazu amepewa hukumu ya kifungo cha nje kwa kesi ya wizi.

Kwa mujibu wa waendesha mashtaka, Nassim alikutwa na kosa la kuiba Tsh 2,671,300 akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258 (1) na 270 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alikiri kosa ambapo mahakama imeamuru atumikie adhabu ya kifungo cha nje cha mwaka mmoja, ikienda sambamba na kurejesha fedha alizoiba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags