Mtazame mtu mwenye kinywa kikubwa duniani

Mtazame mtu mwenye kinywa kikubwa duniani

Miongoni mwa mambo ya kushangaza zaidi hili nalo lipo la mwanamke, Samantha Ramsdell kushikilia rekodi ya kitabu cha kumbukumbu za dunia cha Guinness kwa kuwa na kinywa kikubwa zaidi duniani.

Samantha amewaacha midomo wazi wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti video akionyesha namna pakiti nzima ya vibanzi (crips) inavyoweza kuishia yote kwenye kinywa chake.

Video za Samantha zimeiteka mtandao wa TikTok na kuwashangaza wengi kutokana na ukubwa huo wa kinywa chake.

Kwa mujibu wa Samantha mwenyewe, watumiaji wa mtandao wa TikTok walikubaliana kuwa anahitaji rekodi hiyo baada ya kutazama video zake akipanua kinywa chake na kumtaka ashiriki kwenye mchezo wa kutanua kinywa.

Na kweli aliposhiriki akaibuka kidedea na kutajwa kama mwanamke mwenye kinywa kikubwa zaidi duniani.

Hivi karibuni, Samantha aliwashtua wafuasi wake kwa video yake akionyesha tena namna pakiti nzima ya vibanzi inaweza kutoshea kinywani mwake kwa mkupuo mmoja.

Video yake ilichapishwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Televisheni ya CNN huku wana mtandao wakishtuka kuwa mrembo huyo anaweza kumeza chakula kizima wakati mmoja.

Maoni ya wana mtandao wa Twitter yalikuwa ni mengi huku kila mmoja akionyesha kuduwazwa na baadhi wakitaka kujua kiasi ya chakula ambacho Samantha hula na kuhisi kushiba.

“Kama anaweza kula pakiti nzima kwa wakati mmoja, je, anahitaji pakiti ngapi ili aweze kushiba?” Alihoji mmoja wa watumiaji hao wa Mtandao wa Twitter.

Kwa mujibu wa Samantha, alitambua tangu akiwa mtoto kwamba ana mdomo mkubwa kutokana na picha zake za utotoni alizokuwa akionyeshwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags