Mtanzania ashinda Sh150 milioni kwenye ‘challenge’ ya tajiri wa Russia

Mtanzania ashinda Sh150 milioni kwenye ‘challenge’ ya tajiri wa Russia

Kijana Mtanzania aliyejitambulisha kwa jina la Ernest Thompson, ameshinda Sh150 milioni baada ya kuibuka mshindi wa shindano la mtandaoni ‘challenge’ lililoongozwa na mwanamtandao maarufu na tajiri nchini Russia, Mr Thank You.

Katika shindano hilo la bahati nasibu lililowahusisha washiriki zaidi 500,000 duniani, Ernest alibahatika kushinda gari aina ya Porsche Cayenne baada ya droo kuchezeshwa, hata hivyo alipotafutwa na mwanamtandao huyo aliulizwa anachagua nini kati ya gari au Sh150 milioni?

“Unachagua nini kati ya gari (Porsche Cayenne) au tukutumie fedha (Sh150 milioni)?” aliuliza Mr Thank You, ambapo Ernest alichagua fedha.

Shindano hilo liliwahitaji washiriki kum-follow Mr Thank You pamoja na rafiki zake 50 katika Mtandao wa Instagram kisha majina ya walioshiriki yanaingizwa katika mfumo maalumu wa kumchagua mshindi.

Mwananchi imemtafuta, Ernest ambaye amekiri kushinda fedha hizo huku taratibu za malipo zikiendelea.

“Kwa sasa taratibu zinaendelea za namna ya kupata malipo. Mimi ni mhitimu wa chuo cha Usafirishaji (NIT) na kwa sasa naishi Bagamoyo,”amesema Ernest.

Mwananchi inaendelea kumtafuta ‘Mr Thank You’ kwa ajili ya mahojiano zaidi, licha ya kuwapo baadhi ya watu wakihofia huenda mwanamitandao huyo anafanya hayo kwa ajili ya kupata umaarufu na vitu hivyo anavyoahidi havitekelezi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags