Mtangazaji azua gumzo, ameza nzi akiwa live

Mtangazaji azua gumzo, ameza nzi akiwa live

Mtangazaji nchi Marekani aitwaye Vanessa Welch anayefanya kazi katika kituo cha runinga cha Boston25 amezua gumzo na kuwashangaza wengi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kumenza nzi wakati akiwa kwenye matangazo ya moja kwa moja (live).

Welch wakati akiwa live mdudu mweusi alionekana kwenye kope yake na kuangukia mdomoni kisha akammeza na kuendelea kutoa ripoti, watazamaji walishitushwa na tukio hilo kwani kumeza mdudu kunaweza kumfanya mtu yoyote anyamaze.

Vanessa Welch amefanya kazi ya utangazaji katika runinga ya Boston25 kwa miaka nane akiwa kama mwandishi wa habari na mtangazaji.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags