Msanii mchanga aliye saidiwa na Babu Tale akimbiza You Tube

Msanii mchanga aliye saidiwa na Babu Tale akimbiza You Tube

Baada ya Mh.Babu Tale kuonesha nia ya kumsaidia msanii chipukizi wa muziki wa Bongo Fleva Founder, watanzania pia wameonekana kuungana na Babu Tale katika kuinua kipaji cha kijana huyo mwenye sauti isiyo na mfano.
Kupitia wimbo wa kijana huyo ‘nitatokaje' ambao ndiyo ulimfanya aonekane na kupendwa na wengi umeonesha dhahiri mapokezi ya watu juu ya kijana huyo kwani watu wengi wamefika na kuchungulia kwenye mtandao wa YouTube wa kijana huyo.
Akiwa na jina changa kabisa katika game ya muziki amefanikiwa kufikisha watazamaji milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube ikiwa zimepita siku kumi tu tangu aachie video ya wimbo wake wake.
Maono ya wengi yanaenda kumtazama Founder kama baadhi ya wasanii wanaofaya vizuri kwenye game baada ya kutambulisha wakiwa na umri mdogo kama vile kipindi anatambulishwa #DogoJanja, #Aslay, #YoungD, #BekaFleva.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags