Msako mkali wafanyika kwenye makazi ya Diddy

Msako mkali wafanyika kwenye makazi ya Diddy

Makazi ya nyota wa muziki wa hip-hop, Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami jana Jumatatu , Machi 25, yamefanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.

Uchunguzi huo uliongozwa na mawakala wa Uchunguzi wa Usalama wa Nchi (HSI). Tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili Diddy ni zile zilizoanza kuvuma tangu mwaka jana.

Hata hivyo, katika upekuzi huo, watoto wawili wa kiume wa Diddy, Justin na King Combs, walitiwa mikononi mwa askari.  Jumba la Diddy lililofanyiwa upekuzi ni lile ambalo alizindulia albamu yake ya mwisho mwaka jana (The Love Albam Off the Grid).

Utakumbuka kuwa mpenzi wa zamani wa Diddy, Casandra Ventura, maarufu kwa jina Cassie, aliwahi kumshutumu Diddy kwa kumbaka na kumshambulia mara kwa mara, na kusema alimlazimisha kufanya mapenzi na wanaume mbele yake.

Pia Joi Dickerson-Neal alimshutumu Diddy kwa kumpa dawa za kulevya na kumbaka mwaka wa 1991. Si hivyo tu zipo tuhuma nyingine pia za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili nyota huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags