Mrembo afariki baada ya upasuaji

Mrembo afariki baada ya upasuaji

Mwanamitandao kutoka nchini #Brazil #LuanaAndrede amefariki dunia muda mchache baada ya kufanyiwa Surgery, tukio hilo lilitokea katika Hospitali ya São Luiz huko São Paulo, ambapo Andrade  alifanya upasuaji huo wa urembo.

Kwa mujibu vyombo vya habari inadaiwa kuwa wakati wa upasuaji huo, uliochukua takribani masaa mawili na nusu, mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 29 alipata tatizo la kupumua ghafla, na kusababisha mshtuko wa moyo na mishipa kuziba kupitisha damu.

Aidha hospitali ilitoa taarifa ikidai kuwa upasuaji huo ulisimamishwa baada ya kufanyiwa vipimo vilivyoonesha mvilio kwenye mishipa ya damu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags