Mr Ibu kuzikwa mwezi wa sita

Mr Ibu kuzikwa mwezi wa sita

Marehemu muigizaji kutoka nchini Nigeria John Okafor (62) maarufu kama Mr Ibu anatarajiwa kuzikwa Juni 28, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa na kaka mkubwa wa Mr Ibu, Sunday Okafor, ambapo ameeleza kuwa wameamua kuchelewesha mazishi hayo ili mwigizaji huyo aweze kupewa mazishi ya kihistoria, ambapo atazikwa nyumbani kwake katika mji aliozaliwa wa Amuri, katika eneo la serikali ya mtaa wa Nkanu Magharibi katika Jimbo la Enugu.

Kufuatia na taarifa hiyo muongozaji wa mazishi hayo Mhe. Monday Diamond Ani ameweka wazi kuwa kutakuwa na sherehe ya siku tano ambapo hafla hiyo itaanza Juni, 25 kutakuwa na mechi maalumu, June 26 Usiku wa Mr Ibu ambapo kutakuwa na mishumaa pamoja na kupata burudani ya moja kwa moja.

June 27 kutakuwa na ibada maalumu nyumbani kwao huko Eziokwe Amuri, huku ibada ya mazishi ikifanyika June 28 na sherehe hizo zitatamatika Jumapili June 30 ambapo familia itatoa shukrani kwa kanisa, marafiki na watu wengine waliohudhuria katika hafla zote za siku tano.

Ikumbukwe kuwa Mr Ibu (62) amefariki dunia Machi 2, 2024 wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Evercare iliyopo nchini Nigeria,

Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia filamu zake kama The Collaborator, My Chop Money na nyingine nyingi akiwa na Aki na Ukwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags