Mr ibu afanyiwa upasuaji, Yupo ICU

Mr ibu afanyiwa upasuaji, Yupo ICU

Baada ya muigizaji kutoka nchini Nigeria Mr Ibu kuomba msaada kupitia mitandao ya kijamii ili aweze kuchangiwa kiasi cha pesa kwa ajili ya matibabu, hatimaye muigizaji huyo tayari amefanyiwa upasuaji.

Kupitia ukurasa wa Instagram familia ya muigizaji huyo imetoa taarifa kuhusiana na maendeleo yake kwa kueleza kuwa Mr Ibu amefanyiwa operation tano na sasa anaendelea vizuri katika chumba cha ICU, huku familia hiyo ikitoa shukrani kwa waliotoa mchango.

Taarifa ya maendeleo ya muigizaji huyo inakuja baada ya vyombo vya habari vya udaku nchini humo kudai kuwa Mr Ibu amefariki hospitali akiwa anapatiwa matibabu.

Mr Ibu watu wengi walimtambua kupitia movie zake kama The Collaborator akiwa na Aki na Ukwa, Mr Ibu, My Chop Money na nyingine nyingi.

Ikumbukwe kuwa utokana na maradhi yake aliwahi kudai kuwa huenda yatamsababishia  kukatwa miguu, hata hivyo mwaka 2022, aligundulika kuwa na ugonjwa wa kisukari na figo na alifanyiwa upasuaji katika kituo cha matibabu cha #Zenith #Abuja.


.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags