Mr Focus kutoka kuimba hadi kufanya kazi ya life couch

Mr Focus Kutoka Kuimba Hadi Kufanya Kazi Ya Life Couch

Nikwambie tu zama zimebadilika sana kijana mwenzangu! wakati tulionao sasa kama  ili uweze kutoboa lazima uangalie tofauti na elimu yako je unakitu gani cha ziada?.

It’s first Monday of August bwana  kama kawaida ni siku ya makala zile za kazi, ajira na maarifa na leo namshusha hapa kijana  mwenzio ambaye ni mwanafunzi kutoka Chuo cha IFM jiji Dar es Salaam akiwa anachukua  Bachelor of Accounting mwaka wa tatu.

Peter Asenga maarufu kama Mr Focus, huyu ni kijana ambaye anakitu cha ziada ukiachana na elimu anayoisomea kwa sasa kwani anajihusisha zaidi na kazi ya Life Couch.

Akizungumza na Jarida la Mwananchi Scoop, Mr Focus amefunguka mambo mbalimbali yanayoihusu kazi hiyo na sababu ambazo zimesababisha yeye kujihusisha zaidi na masuala hayo.

Vilevile alisema anajihusisha zaidi na masuala ya kutoa ushauri wa mahusiano pamoja na masuala ya kijamii akidai kuwa kwa sasa jamii inasumbuliwa sana na masuala hayo.

Aidha alisema alianza kazi hiyo tangu akiwa shuleni kipindi cha ‘morning speech’ alikua akifanya shughuli hizo akizungumzia mambo mbalimbali kwenye jamii na kufundisha mambo yatakayowasaidia katika jamii.

Vile vile alisema kuwa alikua akizungumza masuala ya kimaisha, namna ya kuishi na watu vizuri, pamoja na njia gani waweze kufanya kama wanafunzi ili wafikie malengo yao.

Hata hivyo baada ya kuona kazi anazozifanya jamii inazitambua na kuzielewa pia, ndipo alipoamua kufungua Youtube channel yake mwaka jana inayotambulika kwa jina la Mr focus TGD (The Great Dairy) ambayo anaitumia kuweka kazi zake mbalimbali anazozifanya.

Aidha alizungumzia ugumu wa kazi hiyo ambayo anaifanya akieleza kuwa tatizo kubwa ni suala zima la promotion ndio jambo ambalo linamuangusha sana.

“kazi ninayoifanya ni kubwa sana ya kuelimisha jamii hivyo inahitaji nguvu kubwa , lakini pia wadhamini kwangu imekua changamoto pia licha ya kuwa kazi zangu zinawafikia watu wengi”alisema

Matamanio ya Mr Focus siku za usoni

Hata hivyo kijana huyo matamanio yake makubwa hapo baadae anataka kipindi chake cha The great dairy show kije kuwa kipindi kikubwa ambacho watu watakua wanajifunza mambo mbalimbali ya kimaisha na mahusiano.

“Natamani sana kipindi na kazi ambazo nazifanya ziweze kuwa the best hapo siku za usoni lakini pia bila Mungu hata uwe na malengo makubwa kiasi gani hauwezi kufika hivyo namuomba sana yeye anisaidie zaidi lakini najiona mbali baada ya miaka kadhaa” alisema.

Sambamba na hayo Mr Focus anachukua Bachelor of Accounting lakini anaeleza namna anavyoweza kutwist muda wake wa masomo na kazi anayoifanya.

Akizungumzia suala hilo alisema binafsi yake mara nyingi hutumia muda ambao masomo hayajachanganya Chuo ndiyo muda ambao anautumia kuandaa kazi zake.

Vilevile alitoa ushauri wake kwa vijana wenye uhitaji wa kufanya kazi kama anayoifanya yeye akiwataka wasikurupuke kukimbilia kazi hiyo na badala yake wajipange kwanza kifikra kisha waweze kuifikia shughuli hiyo.

“Hii siyo kazi ya kukurupuka, unatakiwa uwe msomaji, uwe na marifa kichwani, ujifunze kupitia youtube kwani wapo watu mbalimbali ambao wanatoa masomo, kusoma vitabu kwa wingi bila hivyo huwezi kufanikiwa kwenye kazi hii kwani inahitaji muda na umakini wa hali ya juu kwa kile ambacho unawaelekeza wengine”alisema.

 Aidha kijana huyo alisema kitu ambacho anajivunia zaidi ni namna watu wanavyotoa comment zao dhidi ya kazi ambazo anazifanya ambapo jamii imemkubali na kusababisha watu wengi kufuatilia kazi zake.

“Najivunia zaidi wazazi wangu ambao wamekuwa wakiniunga mkono na kunisapoti kwa kiasi kikubwa bila kuwasahau ambassadors wangu ambao  najivunia wao wananisaidia kwenye kupiga hatua”alisema

Fahamu Mr focus wapi alianzia kabla ya kufanya kazi ya life couch.

Mr focus safari yake ya maisha katika kazi ilianzia kwenye masuala ya sanaa kwani alikua mwimbaji hapo awali katika sherehe mbalimbali hususani shuleni alikokua akijfunza.

Aidha alisema baada ya kuanzia huko ndipo akili yake ilianza kupanuka zaidi wakati alipokua akijikita katika kusoma masula mbalimbali ya kimaisha.

Kijana huyo tofauti na kazi anayoifanya bado anavipaji vya kutosha tu uikiwemo presenter, Uandishi pia bila kusahau karama yake ya Uongozi aliyobarikiwa na Mungu.

Mr Focus alizaliwa Mkoani Morogoro na amekulia huko na kusoma shule ya Msingi Mapinduzi, Olevel akasoma Kibaha Sec school na advance alisoma Sengrema secondary school iliyopo Mwanza.

Mr Focus ni kijana ambaye anapenda kuwa smart muda wote anazingatia sana suala la usafi.

“Wakati niko shule nilibahatika kupata ukaka Mkuu shuleni kutokana na Usafi wangu niliokuwa nao kiukweli kwenye suala hilo sina utani kabisa napenda sana usafi.

Aiseee!!! Hakika ni makala ya kuzingatiwa na kujifunza zaidi kwa vijana wengine ambao wako  vyuoni na wanaotarajia kujiunga na elimu ya Ngazi ya juu hakikisha hudharau uwezo uliokuwa nao kwani ndiyo funguo yako mbadala wa elimu yako have a nice Monday!!!!!!!!!!!!!!!!!.

 

 

 


Comments 4


 • Awesome Image
  Mr focus Tanzania

  This is fantastic ,Thank you Team #Mwananchiscoop

 • Awesome Image
  Getrude Isaya

  He is very talented all i can say he should live in what he has and always struggle no matter how many challenges he will face and discourage from haters.. Have learnt something and i will be following up more.

 • Awesome Image
  Getrude Isaya

  He is very talented all i can say he should live in what he has and always struggle no matter how many challenges he will face and discourage from haters.. Have learnt something and i will be following up more.

 • Awesome Image
  Vero

  Mr focus may god bless your work as u deserve . ... we are praying for youh to be know world wide through your work.... .

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on Career and skills development every Monday and entertainment, every Friday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include SMARTPHONE and NIPE DILI.


Latest Post