Mr beast aanza kutoa zawadi ya magari

Mr beast aanza kutoa zawadi ya magari

Baada ya mtengeneza maudhui kutoka Marekani, Mr Beast kuahidi kutokla zawadi ya magari 26 kwa mashabiki zake katika siku yake ya kuzaliwa, hatimae mtengeneza maudhui huyo ametoa list ya mashabiki 10 ambao wamejishindia magari hayo.

Kupitia ukurasa wa Instagram Mr Beast ame-share akaunti 10 za Instagram za mashabiki hao walijishidia magari aina ya Tesla huku akiweka wazi kuwa washindi wengine waliobaki atawatangaza jioni ya leo Mei 15, 2024.

Mr Beast alitangaza kugawa magari hayo kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) ambapo aliweka wazi kuwa katika siku yake ya kuzaliwa mwaka huu atatoa magari 26 kwa mashabiki zake ikiwa kama zamadi kwa kuendelea kumsapoti katika kazi zake.

Ikuimbukwe kuwa mtengeneza maudhui huyo alipata umaarufu zaidi na kuishangaza dunia baada ya kuvunja rekodi ya kuzikwa na kutoka akiwa hai ndani ya siku saba.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags