Mourinho anukia Bayern Munich

Mourinho anukia Bayern Munich

‘Kocha’ wa zamani wa ‘klabu’ ya #ASRoma, #Chelsea na #ManchesterUnited, #JoseMourinho anadaiwa kuwa kwenye mpango wa kuifundisha ‘klabu’ ya #BayernMunich kwa msimu ujao.

Inaelezwa kuwa Mourinho ndiyo anapewa nafasi kubwa ya kumrithi ‘kocha’ #ThomasTuchel ambaye tangu kuanza kwa msimu huu Bayern imekuwa kwenye hali mbaya chini ya ‘kocha’ huyo.

Hata hivyo Mourinho ameshafanya makubaliano na ‘mabosi’ wa Bayern na tayari ameshaanza kujifunza hadi lugha ya Kijerumani ikiwa ni maandalizi kabla ya kuanza kazi rasmi.

‘Kocha’ huyo ambaye kwa sasa hana ‘timu’ baada ya kuachana na AS Roma mwezi uliopita amekuwa akihusishwa na ‘timu’ mbalimbali ikiwemo zile za nchini Saudi Arabia.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags