Morgan Freeman akerwa na tamasha la ‘Black history month’

Morgan Freeman akerwa na tamasha la ‘Black history month’

Mwigizaji mkongwe wa Marekani Morgan Freeman amelikosoa tena tamasha la ‘Black History Month’ huku akidai kuwa analichukia sana tamasha hilo.

Morgan wakati akiwa kwenye mahojiano yake na podcast ya Variety ameeleza kuwa tamasha hilo linamfanya meno yake kuwasha kwa hasira.

“Nalichukia sana, utanipa mwezi mfupi zaidi katika mwaka? Na wewe unaenda kusherehekea historia yako, Wazo hili lote hufanya meno yangu kuwasha kwa hasira kwani sio sawa kabisa.

Historia yangu ni historia ya Amerika, hilo ndilo jambo pekee ninalopendezwa nalo katika ulimwengu huu, zaidi ya kutafuta pesa, kuwa na wakati mzuri na kulala vya kutosha.” Amesema Morgan

Hii sio mara ya kwanza kwa mwigizaji huyo kukerwa na tamasha hilo la mwezi wa historia ya watu weusi kwani mwaka jana aliweka wazi kuwa neno ‘Mwafrika Mmarekani’ ni kama ‘tusi’ kwake.

Utakumbuka kuwa tamasha la ‘Black History Month’ huadhimishwa kila mwaka nchini Marekani huku mwaka huu likianza Fabruari 1, 2024 na kutamatika Machi1.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags