Mohamed Swabri: Biashara imeniondoa katika dimbwi la umaskini

Mohamed Swabri: Biashara imeniondoa katika dimbwi la umaskini

Na Aisha Lungato

Niaje it’s another Tuesday natumaini mko pouwaa wanangu wa mwananchiscoop, siku kama ya leo bwana tunakuletea wanafunzi wanaosoma lakini huku wanajishughulisha na biashara ili kukidhi mahitaji yao na kujikimu katika maisha.

Umaskini ni swala ambalo linamfanya kila mwanadamu alie na kupambana katika kufanya kazi au biashara ili kuondokana na umaskini huo.

Vijana wengi walio chuoni wanaamua kujiingiza katika biashara mbalimbali ili waweze kujikimu kimaisha huku wengine wanapenda tu kufanya ujasiliamali.

Huku wengine wanapenda kufanya biashara ili wasiwe tegemezi katika familia na kwa wazazi wao kwa ujumla.

Mohamed Swabri ni mwanafunzi kutoka katika Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye anachukua kozi ya Bsc, Accounting and Finance.

Mwanakaka huyu anajishughulisha haswa na biashara ya kuuza saa na accessories za simu na jina la brand anayo tumia ni blackie inky 26 store.

Swabri anafunguka a kusema biashara hiyo humsaidia zaidi kujikimu katika maisha na kusaidia wazazi kwa ujumla.

KWANINI BIASHARA YA SAA NA ACCESSORUES ZA SIMU

Kama nilivyo sema hapo awali wengi wetu hufanya biashara kuepukana na umaskini na wengine wanapenda kujishughulisha kwa upande wa Swabri anasema “Kwanza binafsi mimi napenda kufanya biashara, na nilipomaliza kidato cha nne nilipata nafasi ya kufanya kazi kama kibarua katika maduka ya ndugu zangu.

“Kuna changamoto nilipitia ikiwemo kulipwa kipato kidogo na kukosa uhuru kitu ambacho kiliniudhi, hivyo nikaona suala la kuajiliwa si zuri ndipo nikaamua kujiajiri mwenyewe” alisema Swabri

Aliongezea kwa kueleza kuwa “Niliamua kuanzisha biashara yangu binafsi kwa sababu maisha yangu kwa ujumla niliopitia ni magumu kwasababu ya umaskini, suluhisho pekee nililo chukua ni kujituma na kuamua kujikita zaidi katika ufanyaji wa biashara”alisema

Waswahili wanasema biashara ni kama mchezo wa kamari  kwamba kuna kupata na kukosa kwa upande wa kupata nikimaanisha faida kijana huyo yeye alifunguka na kueleza faida anazo zipata kupitia biashara hiyo.

Alisema moja ya faida aliyoipata ni kuamini ndani ya jamii jambo linalomrahisishia ufanyaji wa biashara zake hizo kwa kila siku.

“Faida nimepeta kubwa tu, nimekuwa mtu ninayeaminika na watu wa lika lote wakiwemo vijana wenzangu, kwa upande wa kiuchumi nilipofika namshukuru Allah now brand yangu imekuwa kubwa na kuaminika na jamiii kitu kinachopelekea mauzo kuongezeka na biashara kukuwa hatua kwa hatua” alisema Swabri

Changamoto

Alisema moja ya changamoto anazokumbana nazo ni kuwa na mtaji mdogo jambo linalomfanya kushindwa kupokea kazi zigine zinazohitaji bidhaa nyingi.

“Mtaji wangu mdogo na hii inachangiwa na kukosa support yoyote, pia mahitaji ya msingi kwenye biashara ni makubwa yanasababisha nitumie kiasi kikubwa cha fedha kuliko unachoingiza jambo ambalo ni kinyume na sheria ya biashara.

“Jambo hili pia linasababisha biashara yangu kutoendelea kwa muda mrefu sasa lakini pia kuwepo kwa madeni mengi kutoka kwa watu wangu wa karibu ikiwemo ndugu jamaa na marafiki ” alisema Swabri

USHAURI KWA VIJANA WENZAKO

“Ushauri wangu kwa vijana kwanza maisha ni magumu so kama kijana kuna umuhimu wa kujitambua kwa mambo haya, kwanza kujuwa wewe ni nani katika familia na jamii, unataka nini au kuwa nani katika maisha yako.

“Pia kujua ni gani umechukuwa kufanikisha unacho taka au kuwa nani, jiamini jikubali na jitume huku ukitambua kuwa kila kitu kinawezekana kwa uwezo wa Mungu”alisema

Mbali na masomo, kufanya biashara na kazi kila mwanadamu anakile kitu anapenda kutoka moyoni kwa kijana Swabri yeye hupendelea zaidi kucheza mpira wa kikapu, kuangilia mpira wa miguu pia upendo wa kweli na dhati kwa ndugu jamaa na rafiki.

Vijana wengi hupendelea zaidi nyayo za mwanasiasa au mfanyabiashra aliefanikiwa kwa Swabri yeye role model wake ni mfanya biashara mkubwa ndani na nje ya Tanzania amabae ni Said Salim Bakhresa.

Anatamani kuwa kama Bakresa kwa sababu ya ubunifu wake na usubutu wake katika biashara.

“Pia natamani kuwa mfanyabiashara mkubwa ili niweze kutimiza ndoto zangu ikiwemo kubadilisha maisha yangu na ya familia yangu kwa ujumla,” alisema.

Haya haya mdau na mfuatiliaji wa @mwananchischoop funguka hapo chini wewe unatamani kuwa kama nani eeeeh, umejifunza nini kutoka kwa Mohamed Swabri Au tuambie unatamani kufanya biashara gani lakini mazingira hayakuruhusu kwa namna moja ama nyingine usiache kufuatilia magazine ya @mwananchisoop ili uweze kujifunza mbinu mbalimbali za kibiashara.






Comments 8


  • Awesome Image
    Man issa

    Safi sana Kaka mohammed swabri kwa maelekezo fanisi kwetu sisi vijana. MMI binafsi natamani kufanya biashara ya uuzaji wa Kush..!

  • Awesome Image
    Man issa

    Safi sana Kaka mohammed swabri kwa maelekezo fanisi kwetu sisi vijana. MMI binafsi natamani kufanya biashara ya uuzaji wa Kush..!

  • Awesome Image
    Hossam

    I always appreciate what you are doing bro i see ur prosperity future one day you will make it my bro... But behind those there is GOD whose above all never forget to pray... I learnt and ill continue learning from you .. one love demba

  • Awesome Image
    Hossam

    I always appreciate what you are doing bro i see ur prosperity future one day you will make it my bro... But behind those there is GOD whose above all never forget to pray... I learnt and ill continue learning from you .. one love demba

  • Awesome Image

    No time to die my gee

  • Awesome Image

    No time to die my gee

  • Awesome Image
    Shaqifu bashiru

    Mbele mbele yao.. no time to die my gee 🔥 nakuona mbali never give up

  • Awesome Image
    Mrombo

    🔥🔥🔥🔥❤️

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags