Mocco Genius anavyobadilika kama kinyonga kwenye ngoma zake

Mocco Genius anavyobadilika kama kinyonga kwenye ngoma zake

Kawaida ubunifu ndiyo kitu kinachotofautisha mtu mmoja na mwingine katika kazi ya sanaa hasa katika muziki ambapo kila msanii anatamani kuwa bora kuliko mwenzake.

Wapo ambao wamekuwa na desturi ya kujaribu bunifu kadhaa ili kunogesha kazi zao kama vile kubadili miondoko na midundo ya ngoma zao, na katika hilo mwanamuziki wa Bongo Fleva, Idd Mohamed Ngomba 'Mocco Genius' ambaye hivi karibuni ameonekana kubadilisha miondoko ya ngoma zake kwa kufanya muziki wa ‘kompa’ wenye asili ya Asia amesema kilichofanya kubadilika ni kutengeneza utofauti.

“Mimi niliwaza kufanya muziki wa kompa kwa sababu kwanza kutaka kutengeneza utofauti, kuja na kitu ambacho niliona kinaweza kufanya vizuri, japokuwa kweli nilichokuwa nimekiwaza ndicho kilicho tokea.

 "Pia nilikuwa natafuta sound ambayo inaendana na nyimbo zetu, usikiliza kompa ni kama Zuku au kama Bongo Fleva zile za kipindi cha nyuma ndiyo maana unaona kompa ina ladha ile ya nyumbani,” amesema.

Hata hivyo, ameeleza wakati anaanza kutengeneza muziki wa aina hiyo kabla haujawafikia mashabiki alihisi muziki huo utapendwa tu.

“Sababu nyingine nilikuwa nahisi unaweza kupendwa, kweli nilivyofanya watu walipenda, kompa ni muziki ambao unapendwa sana East Africa japokuwa asili yake ni bara la Asia na America nimeufanya Tanzania na wasanii wengine wameupenda najivunia kuwa miongoni mwa watu ambao nimeuanzisha na kuuleta katika Bongo Fleva,” amesema

Mbali na hayo mwanamuziki huyo amezidi kuonesha makali yake ambapo hivi karibuni ametoa wimbo wa ‘Mar Gaya’ ambao una mahadhi ya Kihindi.

“Wimbo wa Mar Gaya umeongelea zaidi mahusiano ambapo nime-mix na Asian style kama vile ambavyo inaonekana kuna maneno ya Kihindi na kuna baadhi ya ala ya muziki wa kihindi, lakini yote ni kwenye kutafuta tofauti.Nimefanya kompa mfululizo kama nyimbo tano kwa hiyo nimeamua nilete kitu cha tofauti tena,” amesema.

Pia amedai aliamua kwenda na mahadhi ya Kihindi kwenye wimbo huo kwa sababu aliona akifanya kwa namna hiyo atafikisha ujumbe vizuri.

“Kwenye wimbo wa Mar Gaya niliamua nije tofauti kwa sababu kila mtu anaimba nyimbo za kuumiza so niliamua kuja na kitu ambacho kitawagusa watu wengi,” amesema

Wimbo huo ambao una siku ya sita tangu utoke umepata watazamaji elfu hamsini na mbili kwenye mtandao YouTube.

Mocco ameongezea kwa kusema anatamani kufanya muziki ambao unakuwa tofauti lakini mzuri na ladha ionekane.

Mwanamuziki huyo mpaka sasa tayari amefanya wimbo kama ‘Mchuchu’ aliomshirikisha Alikiba, ‘Mi Nawe’ aliomshirikisha Marioo, ‘Hell’, ‘Yamenishika’, ‘Single’  ‘Nikilala’, Nipe, ‘Nakupenda’ na ‘Mar Gaya’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post