Mmiliki wa maduka China aruhusu likizo kwa wafanyakazi wasio na furaha

Mmiliki wa maduka China aruhusu likizo kwa wafanyakazi wasio na furaha

Manzilishi na mwenyekiti wa maduka ya rejareja ‘Pang Dong Lai’ kutoka China aitwaye Yu Donglai, ameanzisha likizo kwa wafanyakazi wake wenye msongo wa mawazo na wasio na furaha.

Sera hii mpya inawaruhusu wafanyakazi kuchukua siku ya mapumziko kila wanapohisi kukosa furaha au kuwa na msongo wa mawazo, bila kuhitaji idhini kutoka kwa uongozi.

Bwana Yu amechukua hatua hii kwa lengo la kuboresha uwiano kati ya kazi na maisha binafsi ya mfanyakazi huku akiamini kuwa biashara inayoongozwa na watu wenye furaha inakuwa ni biashara yenye afya na endelevu.

Sera hii pia inajumuisha kupunguzwa kwa muda wa kazi hadi saa saba kwa kila mfanyakazi na faida kubwa za likizo ya mwaka.

Yapi maoni yako kwenye hili






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags