Mlinzi afukuzwa kazi, Muziki wamponza

Mlinzi afukuzwa kazi, Muziki wamponza

Mlinzi Calvin Denker aliyepata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii baada ya video yake kusambaa akiimba wimbo wa msanii Taylor Swift, wakati akiwa lindo kwenye tamasha alilokuwa akitumbuiza Taylor, afukuzwa kazi.

Kufuatia video hiyo iliyosambaa mlinzi huyo amefukuzwa kazi kwani HR wake aliamini kuwa hakuwa makini katika kazi yake ya kulinda usalama badala yake mawazo yote yalikuwa kwa mwanamuziki huyo aliyekuwa jukwaani kwenye ziara yake ya Eras.

Video ilisambaa baada ya mashabiki waliyokuwa kwenye tamasha hilo kumrekodi mlizi huyo aliyekuwa akilinda kwenye tamasha akiimba mistari ya Taylor mwanzo mwisho, ambaye kwa wakati huo alikuwa jukwaani akitumbuiza.

Mlinzi huyo anadai kuwa kufukuzwa kwake kazi hakumuumi na wala hajutii kwani amepoteza kazi lakini amepata mashabiki wapya wenye mapenzi ya dhati katika mitandao ya kijamii ambao ataanza kufanya nao kazi kupitia mitandao hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags