Mkubwa Fella atilia mkazo msako wa wasanii mateja

Mkubwa Fella atilia mkazo msako wa wasanii mateja

Ikiwa ni siku moja  tangu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo kuwaonya wasanii wanaotumia na kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya , zikiwamo cocaine, heroin na bangi. Meneja wa mwanamuziki, Naseeb Abdul (Diamond), Said Fella ametilia mkazo suala hilo na kusema kuwa wasanii hao wachukuliwe hatua.

Fella alizungumza na gazeti la Mwananchi na kueleza kuwa,

“DCEA iliyoyaona imeyaona au kama kuambiwa kaambiwa, ombi langu ni atumie vyombo vyake kwa uzuri (Aretas Lyimo) ili mradi afanikishe hili, Watanzania wengi huwa tunapenda kunyooshea vidole watu, wengine wakifanikiwa wapo wanaotaka wasifanikiwe. Kikubwa ni kuwa na vyanzo vya uhakika kwenye hili,” alisema Fella, maarufu kama Mkubwa Fella.

Lyimo alisema kuwa wana orodha ya wasanii wanaotumia dawa hizo ambao wamewapa muda wa kujirekebisha kabla ya kuwashughulikia baada ya maabara ya mamlaka kukamilika.

Huku akiwaonywa wasanii wanao hamasisha jamii kwa kutumia nyimbo zao, mavazi yao yanayo kuwa na majani ya bangi, maneno na matendo yao yanayo onesha dhahiri kutumia dawa za kulevya kuacha mara moja.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags