Mkongwe avunja rekodi ya kunyanyua vitu vizito

Mkongwe avunja rekodi ya kunyanyua vitu vizito

Brian Winslow mzee wa miaka 86 kutoka Derbyshire amevunja rekodi za dunia na kitaifa katika shindano lake la mwisho la  kunyanyua vitu vyenye uzani mkubwa.

Katika jaribio lake la kwanza mzee huyo alinyanyua kilo 75 katika mashindano ya Jumuiya ya Kuinua vitu vizito Uingereza (BDFPA) yaliyofanyika Machi 18, 2023 na kuboresha tena rekodi hiyo kwa kuinua kilo 77.

Winslow sasa anashikilia Rekodi za Uingereza na Dunia katika kitengo cha kilo 60 kwa washindani wa kiume wenye umri wa miaka 85 hadi 89, kulingana na BDFPA.

Mzee huyo ambaye alianza kunyanyua vitu vizito akiwa kijana alipokuwa akifanya kazi kama mhudumu kusini mwa Devon, alifunguka na kueleza kuwa

 “Nimefurahia Kunyanyua uzani ni sehemu kubwa ya maisha yangu, pamoja na watoto wangu na wajukuu nitaendelea kwa muda kadiri mwili utakavyoniruhusu, siku zote kupata rekodi moja au mbili” amesema Brian






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags