Mke wa Tory Lanez adai talaka

Mke wa Tory Lanez adai talaka

Mke wa rapa kutoka Marekani Tory Lanez, Raina Chassagne anadaiwa kudai talaka, ikiwa zimebaki siku chache kutimiza mwaka mmoja katika ndoa yao waliyoifunga mwaka 2023.

Kwa mujibu wa Tmz Raina amewasilisha ombi la talaka Mahakamani akidai kuwa sababu kuu ya kufanya hivyo ni kutokuwa kwenye maelewano mazuri na mumewe jambo linalopelekea kuwa na tofauti zisizo suluhishika.

Katika hati hizo zilizofikishwa Mahakamani Raina pia ameomba haki ya malezi ya mtoto wao aitwaye Kai (7) wakati baba wa mtoto huyo akiendelea kutumikia kifungo chake cha miaka 10 jela.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walifunga ndoa ya siri Juni 25, 2023 kipindi ambacho Lanez anakabiliwa na mashitaka ya kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake.

Rapper huyo alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela mwezi Agosti mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga risasi nyota wa hip-hop Megan Thee Stallion.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post