Mke wa Obama aikubali albamu ya Beyonce

Mke wa Obama aikubali albamu ya Beyonce

Baada ya albamu ya mwanamuziki Beyonce iitwayo ‘Cowboy Carter’ kutajwa na mashabiki kuwa ndiyo albamu bora ya mwaka 2024, sasa imemfikia mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama ambaye ameonesha hisia tofauti katika albamu hiyo.

Michelle Obama kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share ujumbe wa kumpongeza mwanamuziki huyo haswa kwenye wimbo wake uitwao ‘Ya Ya’ ambao umeelezea zaidi kuhusiana na upigaji kura unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini humo.

Aidha Michelle amemtaja Beyonce kuwa ndiye mwanamuziki aliyevunja rekodi katika matumizi ya historia baada ya kutumia muziki na kipaji chake kupaza sauti katika masuala ambayo ni muhimu kwenye Taifa lao yakiwemo uchaguzi.

Wimbo huo ‘Ya Ya’ ambao mwishoni kabisa Queen Bey amesema kuwa ‘Marekani inahitaji kuweka imani na kupiga kura’ siku chache zilizopita uliripotiwa kuwa uliandikwa Jay-Z ambaye ni mume wa Beyonce.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags