Mke wa aliyekuwa rais wa Gabon atupwa gerezani

Mke wa aliyekuwa rais wa Gabon atupwa gerezani

Baada ya kutumikia kifungo cha nyumbani tangu Agosti 30, 2023, hatimaye mke wa Rais wa zamani wa Gabon, Sylvia Bongo ametupwa jela katika gereza la Libreville, Oktoba 10 kwa madai ya ubadhirifu wa fedha za umma, kupola, mali za wizi na kughushi nyaraka.

Taarifa hiyo imetolewa na wakili wake François Zimeray siku ya jana Octoba 12 kwa vyombo vya habari kuwa mteja wako huyo aliingizwa gerezani siku ya jumatano jioni baada ya jaji kumsikiliza kwa muda mrefu huku wakili huyo amenukuliwa akisema Sylvia amefungwa kwa utaratibu usiyo halali.

Wakati hayo yanajiri mtoto wao, Noureddin Bongo pia amefunguliwa mashitaka ya rushwa, ubadhirifu wa fedha na kuwekwa kizuizini kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags