Mjamzito achomwa kisu na mzazi mwenzie

Mjamzito achomwa kisu na mzazi mwenzie

Binti mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Dumila, wilaya ya kilosa mkoani Morogoro amejeruhiwa na mzazi mwenzake ikielezwa alimgomea kwenda kulala naye licha ya wawili hao kuwa wameachana.

Mwenyekiti wa kitongoji cha njia panda, sadick kazikula amesema wakati tukio linatokea walikuwa kwenye ulinzi na waliposikia kelele walifika eneo la tukio lakini mtuhumiwa alikuwa ameshakimbia, hivyo walimchukua majeruhi na kumpeleka hospitali.

Nae mganga mfawidhi hospitali ya mtakatifu joseph, dokta manyele kapongo, amesema majeruhi anaendelea vizuri kwa kuwa kisu hakikufika kwenye utumbo na mfuko wa uzazi,

Mfuko wa uzazi haujaathiriwa na jeraha hilo lakini Msichana ana ujauzito wa wiki saba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags