Mtoto wa Mfalme wa Pop Michael Jackson, anayefahamika kama Price Jackson afichua tatizo la ngozi alilokuwa nalo baba yake na kukanusha kuwa MJ hakuwa anafanya makusudi kubadilisha ngozi yake.
Price Jackson wakati akifanya mahojiano kwenye #HotboxinPodcast amedai kuwa baba yake alikuwa na tatizo la ngozi linalofahamika kama Vitiligo ambalo lilimfanya asijiamini kuhusu muonekano wake, ndipo katika hatua ya kuponya tatizo hilo kulipelekea MJ aweze kupoteza rangi yake ya awali bila kukusudia.
Kijana huyo wa MJ ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 26, amedai kuwa wakati akiwa mdogo baba yake alikuwa akimuelezea kila mara kuhusiana na tatizo hilo la ngozi lililokuwa likimkabili, ambalo hata baada ya kifo chake lilikuwa kwenye ripoti ya uchunguzi wa maiti.
Aida akaendelea kwa kudai mengine yote yanayoendelea kuhusu baba yake ni uvumi tu bali kilichosababisha ngozi ya baba yake kubadilika ni mapambano yake dhidi ya ugonjwa huo wa Vitiligo.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa kabla ya maoni ya mtoto huyo kuhusu ngozi ya baba yake, Michael Jackson mwenyewe mwaka 1993 wakati akifanya mahojiano na Oprah Winfrey, aliwahi kukanusha madai ya yeye kubadili ngozi yake.
MJ alimwambia Oprah, kuwa yeye ni mweusi na anajivunia kuwa mmarekani mweusi na anajivunia rangi yake, na kueleza kuwa ana ugonjwa wa ngozi ambao ndiyo chanzo cha ngozi yake kuharibika, na alidai watu anaumizwa na watu wanaotunga hadithi dhidi yake, kuwa hataki kuwa mweusi bila kufahamu tatizo analopitia, na akadai si yeye hata baadhi ya watu kwenye familia yake wanapitia changamoto hiyo akiwemo baba yake Joe Jackson.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BuridikaNasi
Leave a Reply