Miss Tz 2022 azungumzia tetesi za warembo kuuzwa kwa wanaume

Miss Tz 2022 azungumzia tetesi za warembo kuuzwa kwa wanaume

Miss Tanzania 2022, Halima Kopwe ambaye aliiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo duniani amekanusha tetesi zinazodai kuwa waandaaji wa shindano la urembo Miss Tanzania huwauza washiriki kwa wanaume.

Akizungumza na Mwananchi, Halima amesema maneno hayo ni uvumi na propaganda za kwenye mitandao ya kijamii lakini katika uhalisia hakuna kitu kama hicho.

"Hizo ni propaganda kuwa waandaaji wanauza warembo, naona hakuna uelewa kwa kiasi kikubwa natamani hata ningekuwa nafanya 'reality show' ili watu waone vitu vinavyoongelewa mtaani siyo vinavyotokea kambini.

"Sisi tunakaa kambini na wasichana hawatakiwi kuonana hata na ndugu, jamaa au marafiki kuna Matroni, Pratron na Trainers tu,"amesema.
Hata hivyo, amesema nchini bado tasnia ya urembo haijatiliwa mkazo kama kwenye mataifa mengine.

"Kwa Tanzania bado tasnia ya urembo haijachukuliwa 'siriazi' tuna warembo wazuri sana lakini hawalipwi vizuri kwa sababu Watanzania bado hatujachukulia hiyo kama sanaa,"amesema.

Aidha alifunguka kuwa ingetokea akawa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo angezingatia masuala ya urembo.

Utakumbuka kuwa Halima aliwabwaga warembo 20, aliopanda nao jukwaani katika fainali ya shindano la kumpata mrembo wa Tanzania 2022 na kumfanya ajishindie zawadi ya gari aina ya Mecedez Benz yenye thamani ya Sh 40 milioni na kitita cha Sh 10 milioni.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post