Mikataba ya siri, Chanzo kesi za unyanyasaji wa kingono kuibuka

Mikataba ya siri, Chanzo kesi za unyanyasaji wa kingono kuibuka

Kumekuwa na wimbi la kufufuka kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono walizowahi kufanyiwa baadhi ya wanawake na mastaa wakubwa duniani, kama zilivyoibuka tuhuma kwa P Diddy, R Kelly, Jermaine Jackson,Vin Diesel na wengineo.

Kutokana na matukio haya kuibuka baada ya kutendeka kwa miaka mingi Master J akizungumza Mwananchi Scoop anasema matukio kama hayo yamekuwa yakiibuka sasa hivi huenda kutokana na makubaliano ya mtenda na mtendewa, kwani wapo baadhi ya watu ambao huingia mikataba ya kufichiana siri hata wakifanyiwa unyanyasaji hivyo basi endapo mikataba ya kukaa kimya ikiisha ndipo huibuka na kufungua kesi.

Master amesema mikataba ya aina hiyo hata Tanzania ipo wapo wasanii wanawafanyia wanawake vitendo vya kingono na kisha kuwalipa kwa mikataba ya kutozungumza kitu juu ya walichofanya.

Aidha kwa upande wake mwanamuziki Mwasiti anasema watoto wengi wa kike wananyanyasika lakini hawana sehemu ya kusemea  hivyo siku wakipata sehemu ndiyo hufunguka na kutokea kama yaliyowakuta P Diddy na R. Kelly.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags