Michelle Obama azindua kampuni ya chakula na vinywaji

Michelle Obama azindua kampuni ya chakula na vinywaji

Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Michelle Obama ametangaza na kuzindua kampuni yake ya vyakula na vinywaji vyenye afya ambayo ameianzisha ili kuwapa wazazi bidhaa bora na zenye ladha nzuri kwa ajili ya watoto wao.

Michelle Obama amezindua kampuni hiyo iitwayo “PLEZi Nutrition” ambapo bidhaa yake ya kwanza ni juisi ya matunda hususani kwa watoto iliyo na sukari chini ya 75% kuliko wastani wa juisi za matunda zenye 100% ya sukari.

Bidhaa hiyo ya PLEZi tayari inapatikana katika baadhi ya maduka ya rejareja huko Marekani  huku kampuni ikipanga kusambaza vitafunio na vinywaji vingi zaidi katika miaka michache ijayo ikilenga kupunguza kiwango cha sukari

ili kuwatengezea Watoto mazingira ya kutotamani vitu vyenye sukari nyingi kwa ajili ya kuboresha afya yao.

Lakini pamoja na hayo itakumbukwa Michelle Obama katika nafasi yake wakati akiwa Mke wa Rais aliongoza kampeni iitwayo “Let’s Move” ambao ni mpango unaolenga kukomesha hali ya unene wa kupindukia kwa Watoto,

Mafanikia ya kampeni hiyo yalikuwa makubwa kutokana na kupitishwa kwa sheria ya watoto nchini Marekani ambayo iliunda viwango vya lishe vya shirikisho kwa chakula cha mchana ambacho watoto hupatiwa mashuleni.

Moja ya chombo cha habari Marekani ililiripoti hapo awali kwamba vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa Marekani vilisema kiwango cha unene wa kupindukia kilipungua kwa asilimia 43 miongoni mwa watoto wadogo wenye umri wa miaka miwili hadi minne

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Michelle aliandika kuwa “Wasichana wangu walipokuwa wachanga, hakuna chaguo lililo kuwa muhimu zaidi kuliko ubora wa chakula na vinywaji nilivyowapa. Mara kwa mara nilijikuta nikitamani kuwe na chaguzi zaidi za afya zinazopatikana kwa akina mama kama mimi. Hiyo ni sehemu kubwa ya sababu iliyonifanya nifanye kazi kwa bidii kama Mama wa Kwanza kusaidia watoto na familia kula chakula bora na kuishi maisha yenye afya” amesema Michelle Obama

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags