Michelle Obama akanusha kugombea urais 2024

Michelle Obama akanusha kugombea urais 2024

Baada ya kuzuka tetesi kuhusiana na mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama kutaka kugombea Urais 2024, Michelle amekanusha tetesi hizo kupitia ofisi yake siku ya jana Jumanne Machi 5.

Ofisi hiyo imelithibitisha hilo kwa kueleza kuwa Michelle hatogombea Urais kwani kwasasa ameamua kujikita kumuunga mkono Rais Biden katika kampeni zake ili kufanikisha achaguliwe tena.

Uchaguzi nchini Marekani unatarajiwa kufanyika Novemba 5, 2024, na mpaka sasa waliojitokeza kugombea Urais ni pamoja na Biden ambaye yupo madarakani na Donald Trump.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags