Michael Jordan aingia kwenye orodha ya Forbes ya matajiri 400

Michael Jordan aingia kwenye orodha ya Forbes ya matajiri 400

Nyota mashuhuri wa mpira wa kikapu Michael Jordan anadaiwa kuingia kwenye orodha ya watu 400 matajiri zaidi Marekani ambao huandikwa kwenye orodha inayoheshimika ya Forbes 400 .

Mchezaji huyo wa zamani wa Chicago Bulls anadaiwa alipata dola 94 milioni na alikuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye ligi’ mwaka 1997 na 1998, lakini mapato yake makubwa yalitoka nje ya uwanja.

Moja ya mambo muhimu yaliyochangia Jordan kujumuishwa kwenye orodha hiyo ya matajiri ni uuzaji wake wa hivi karibuni wa ‘timu’ ya Charlotte Hornets, timu ambayo aliipata mwaka wa 2010.

Kwa hiyo kupitia uuzaji wa timu hiyo inaelezwa amepata takribani $2.4 bilioni ambazo zinaongeza kiwango cha utajiri wake hadi kufikia utajiri wa $3 bilioni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags