Michael Jackson apata wakufanana naye

Michael Jackson apata wakufanana naye

Kutokana na kuwepo kwa mpango wa kutengenezwa  filamu ya mfalme wa Pop Michael Jackson (MJ) huku akisakwa mtu ambaye atafanana na kuwa na miondoko kama msanii huyo, hatimaye mtu huyo amepatikana ambaye ni Mpwa wa MJ aitwaye, Jaafar Jackson.

 

Kwa mujibu wa muongozaji  Antoine Fuqua na mtayarishaji Graham King wa filamu hiyo, wameeleza kuwa japo Jaafar anauwezo mdogo katika uigizaji lakini ndiye mtu pekee ambaye amebeba uhusika wa MJ ipasavyo, hivyo wanafuraha sana kumfufua mwanamuziki huyo katika tasnia ya uingizaji.

 

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Jaafar ame-share picha ambazo zinamuonesha akiwa kwenye mapozi ya MJ akiambatanisha na ujumbe ukieleza kuwa ni furaha na heshima kubwa kwake kutekeleza uhusika wa mjomba wake Michael.

 

Filamu hiyo ya ‘Michael’ ilipangwa kuazwa kurekodiwa mwaka 2023 lakini kufuatiwa na changamoto, imeanza kurekodiwa mwishoni mwa Januari 2024 huku ikitarajiwa kuachiwa rasmi Aprili 18, 2025.

 

Jaafar Jackson (25) ni mwanamuziki na dansa ambaye alianza kuimba rasmi akiwa na umri wa miaka 12, na kujulikana rasmi mwaka 2019 baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Got Me Singing’, huku wimbo wake wa mwisho ameachia jana Februari 14 uitwao, ‘Rebirth of Michael’.

Ikumbukwe kuwa Michael Jackson alizaliwa mwaka 1958 na kufariki dunia mwaka 2009. Alitamba na nyimbo zake kama vile Smooth Criminal, Thriller, Will You Be There.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags