Miaka 9 jela kwa kuiba vibawa vya kuku

Miaka 9 jela kwa kuiba vibawa vya kuku

Mwanamke mmoja aitwaye Vera Liddell (68) ambaye pia alikuwa ni mkurugenzi wa huduma za chakula katika Shule ya Illinois, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa baada ya kukiri kuiba mabawa ya kuku wenye thamani ya $1.5 milioni.

Kwa mujibu wa mtandao wa Wealth umeeleza kuwa mwanamama huyo alijihusisha katika wizi huo kwa takribani miaka miwili huku ikigundulika kuwa aliagiza zaidi ya maboksi 11,000 aliyoyalipia kiudanganyifu.

Mpango huo uligunduliwa wakati wa ukaguzi wa kawaida, ambapo meneja wa biashara wa wilaya aliona ongezeko kubwa la bajeti katika idara ya huduma za chakula, ndipo ikigundulika kuwa Liddell alikuwa akifanya mchezo huo.

Hata hivyo mamlaka iliweka wazi kuwa vipande hivyo vilikuwa ni kwa ajili ya kuvisambaza kwa wanafunzi kipindi cha janga la Corona. Aidha Liddell alikabiliwa na mashitaka ya wizi na kuendesha biashara ya uhalifu toka Januari 2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags