Mgonjwa aiba ambulance iliyombeba na kwenda kulewea

Mgonjwa aiba ambulance iliyombeba na kwenda kulewea

Hahahah! Make hapa kwanza nchekee, aliesema ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni wala hakukosea, basi bwana Matthew Checko mwenye umri wa miaka 47 ameiba ambulance iliombeba alipokuwa anapelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu na kwenda nayo kulewea.

Tovuti ya Daily News nchini humo imesema baada ya Checko kufikishwa hospitalini hapo alitoka kinyemera kisha kuliiba gari hilo lililokuwa limeegeshwa na funguo zikiwa ndani na kutimka nalo.

Taarifa ya Polisi imeeleza tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi, Machi 30 ambapo gari hilo lilikuwa limeegeshwa nje ya hospitali ya Mlima Sinai Morningside ambapo gari hilo  halikuwa limefungwa wala hakukuwa na mtu ndani ambapo Checko alitoroka nalo majira ya saa kumi na moja alfajiri.

Polisi nchini humo walifuatilia gari hilo kupitia kifaa cha GPS na kufanikiwa kumkamata. Aidha mtuhumiwa huyo ameshtakiwa kwa makosa ya ulaghai, kumiliki mali ya wizi na kuendesha gari akiwa amelewa






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags