Mgombea wa useneta auawa kwa kupigwa risasi

Mgombea wa useneta auawa kwa kupigwa risasi

Mgombea wa kiti cha useneta  Oyibo Chukwu kutoka nchini Nigeria ameuawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuchomwa moto na washambuliaji, alipokuwa akitoka kwenye mkutano wa kampeni katika jimbo la kusini la Enugu.

Shambulio dhidi ya mgombea huyo wa Chama cha Labour lilitokea siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu wa Jumamosi ambao unaelezwa kuwa uchaguzi wenye ushindani mkubwa zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka 24.

Wasaidizi waliokuwa pamoja naye pia waliuawa kwa kupigwa risasi kabla ya gari lao kuchomwa moto huku miili ikiwa ndani, vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti

Chama hicho cha Labour hakijatoa maoni yoyote kuhusu shambulio hilo, lakini mgombea wake wa urais Peter Obi amekuwa akiwataka wafuasi wake kupiga kura kwa usahihi, kwa amani na matumaini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post