Mfugaji wa nyoka auliwa na nyoka aliemlea toka yai

Mfugaji wa nyoka auliwa na nyoka aliemlea toka yai

Katika taarifa nyingine ya kusikitisha na kushangaza kijana mmoja alie tambulika kwa majina David Riston mwenye wa miaka 49 aliyekuwa amewafuga takribani ya nyoka 100 amepatikana amefariki nyumbani kwake katika jimbo la Maryland huko nchini Marekani.

Maafisa wa polisi katika jimbo hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa kifo cha David kimetokana na kung’atwa na nyoka aliekuwa anamfuga mwenyewe aliweza kumjeruhi  kwa bahati mbaya.

Pamoja na hayo maafisa wa upelelezi wa Maryland walisema kuwa mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa pamoja na nyoka 124 nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa  moja ya chombo cha habari huko Marekani imethibitika nyoka hao wakiwemo cobra wenye sumu kali, chatu wa Burma mwenye urefu wa futi 14 na black mamba ambao walisababisha zoezi la kuuokoa mwili wa David ambae ndio  mmiliki wao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags