Mfanyabiashara ashtakiwa kwa kuwasilisha nyaraka za uongo TRA

Mfanyabiashara ashtakiwa kwa kuwasilisha nyaraka za uongo TRA

Jackson Mali mfanyabiashara kutoka mkoani Songwe amefikishwa mahakamani akidaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo TRA, kwa kujihamishia umiliki wa magari kinyume cha sheria.

Pia anadaiwa kuendesha biashara za ukopeshaji fedha bila kusajiliwa, kitendo ambacho ni kosa la jinai ambapo alitiwa hatiani na kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoani Mbeya.

Aidha mshtakiwa amekana mashtaka yote na amepelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana na shauri limepangwa kuendelea kwa hatua ya kuanza kusikilizwa mei 22, 2023.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags