Nchini India ukiwa mwizi sana unaitwa ‘Natwarlal’, kwa sababu ni jina la mwanaume mmoja kati ya wezi wakubwa kuwahi kutokea kwenye nchi hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Indian Times, Natwarlal alizaliwa mwaka 1912 nchini humo, aliwahi kuuza jengo la bunge la India na jumba la makumbusho la ‘Taj Mahal’ ambayo kivutio kikubwa cha utalii nchini India.
Mwanaume huyu ambaye jina lake kamili ni Mithilesh Kumar Srivastava anadaiwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kughushi nyaraka na saini ambazo ndiye alikuwa akizitumia katika kufanya utapeli wake.
Hata alipokuwa analiuza bunge aliigiza kama yeye ni mfanyakazi wa serikalini na akawalaghai hadi wabunge ambao walihusika kwenye mchakato huo.
Inaelezwa kuwa mwanaume huyo pesa alizokuwa anazipata alikuwa akitumia kwenda kutoa misaada kwenye kijiji alichozaliwa cha Bangra.
Inaelezwa kuwa aliwahi kukamatwa zaidi ya mara tisa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 113 jela lakini mara zote alitoroka, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1996 ambapo alikuwa na umri wa miaka 84, akiwa anatembelea kiti cha matairi mawili lakini bado akafanikiwa kuwakimbia polisi na tangu hapo hakujulikana alienda wapi ingawa kaka yake anadai alifariki mwaka huo huo, huku mwanasheria wake anadai alifariki mwaka 2009.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply