Mfahamu mwanamke anayepiga miluzi kwa kutumia pua

Mfahamu mwanamke anayepiga miluzi kwa kutumia pua

Lulu Lotus mzaliwa wa Mississauga nchini Canada ambaye anashikiria rekodi ya kuwa binadamu anayeweza kutumia pua kupiga miluzi inaoendana na sauti za nyimbo mbalimbali, anaendelea kuupiga mwingi kupitia mitandao ya kijamii kufuatiwa na kipaji hicho.

LuLu aligundua kipaji chake kwa mara ya kwanza alipokuwa na umri wa miaka saba, alikuwa akifanya hivyo kwa walimu na wanafunzi wenzake kwa lengo la kuwafurahisha huku akiweka wazi kuwa anaweza kupiga mluzi na kuimba kwa kutumia misuli yake ya koo kuthibiti hewa inayotoka kwenye pua.

Ikiwa ataacha mdomo wazi, sauti itatoka kinywani badala yake hufumba mdomo na sauti hutokea puani, licha ya hayo Lulu anatamani mwanaye kuja kupiku rekodi yake anayoendelea kuishikiria ya kuwa mwanadamu wa kwanza kutumia pua kuimba kwa kupiga mluzi. Hata hivyo amegundua kuwa mtoto wake anakipaji kama chake.

Lulu Lotus alivunja rekodi ya ‘Guinness World Records’ Juni 3 mwaka 2022 baada ya kuwashangaza wengi katika tamasha la Aercoustics Engineering Ltd. Lililofanika Mississauga, ambapo waandaaji walitumia mita ya kiwango cha sauti cha Brüel & Kjær 2250, kugundua kuwa ilikuwa ni sauti yake kweli ndipo akaingia katika kitabu cha Guinness.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags